Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuna uwezo wa kutokomeza ndoa za utotoni Malawi- Chifu Kachindamoto

Tuna uwezo wa kutokomeza ndoa za utotoni Malawi- Chifu Kachindamoto

Pakua

Nchini Malawi karibu nusu ya wasicha wote huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18 na hivyo hukosa elimu, hukabiliwa na ndoa za utotoni na pia athari nyingine kubwa za kiafya ikiwemo fistula na hata kupoteza maisha kutokana na kujifungua wakiwa na umri mdogo.  Sasa wanaharakati wamelivalia njuga sula hilo ambalo mzizi wake ni mila na desturi. ANOLD KAYANDA anatupasha zaidi

Ni sauti ya mmoja wa wanaharakati wakubwa wa kupigania haki za wasichana Malawi Chifu Teresa Kachindamoto kwa mtoto wa misho kati ya watoto 12 aliyebahatika kwenda kusoma ng’ambo, dhamira yake imekua kuhakikisha kila msicha nchini humo anapata elimu na kutopitia ndoa za utotoni.

Duniani kote wasichana zaidi ya milioni 700 walio hai hii leo wameolewa kabla ya kutimiza miaka 18 na wengi kuwa mama wangali watoto akisema kuwa, “nilirejea nyumbani nikiwa bado na mashaka endapo niko tayari kubeba jukumu hili, na wakati nikipita mtaani katika kiwanjani nikaona wasichana wakiangalia mpira wa miguu, kulikuwa na moja hasa aliyenigusa alikuwa amebeba mtoto mgongoni, nikaenda kuongea naye na akaniambia mtoto ni wake nilishutaka sana pale  aliponitajia umri wake alikuwa na miaka 13”

Audio Credit
Flora Nducha/Arnold Kayanda
Audio Duration
2'12"
Photo Credit
UN Women