30 Mei 2019

30 Mei 2019

Hii leo tunaanzia Ujerumani ambako Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres amepokea tuzo ya mwaka huu ya Charlmangne inayopatiwa watu wanaochangia muungano wa Ulaya, ambapo mwenyewe kasema tuzo hiyo si yake bali ya wanawake na wanaume wa Umoja wa Mataifa wanaochangia kusongesha maadili ya Ulaya ulimwenguni kote. Tunaangazia pia akili bandia ambako Tanzania Dokta Elsa ameleta mafanikio makubwa kwenye huduma ya afya vijijini, na huko Malawi, mwanamke mmoja asimulia iweje alichaguliwa kuwa chifu na sasa anasongesha haki za watoto wa kike kupata elimu. Makala tunabisha hodi nchini Uganda kunani? na mashinani kijana mjasiriamali muuza miche ya mbegu za mihogo asema kilimo kinalipa! Mwenyeji wako leo ni Flora Nducha.

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
11'46"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud