Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwazi kwenye ununuzi wa dawa ni muhimu kusongesha afya kwa wote

Uwazi kwenye ununuzi wa dawa ni muhimu kusongesha afya kwa wote

Pakua

Mkutano wa Baraza Kuu la shirika la afya duniani, WHO umefikia ukingoni leo kwa kupitisha azimio linalohusu kuboresha suala la uwazi wa masoko ya dawa, chanjo na bidhaa nyingine za afya katika jitihada za uwezekano katika kurahisisha upatikanaji bidhaa hizo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Washiriki wa mkutano huo ulioanza Geneva, Uswisi tarehe 20 mwezi huu, wamepitisha azimio hilo ambalo linazitaka nchi wanachama kubadilishana taarifa kuhusu bei kamili ya dawa inayolipwa na serikali na wanunuzi wengine wa bidhaa za afya. 

Halikadhalika linaliomba shirika la afya duniani WHO kuunga mkono jitihada za kuwepo uwazi na kufutilia athari za uwazi katika uwezo wa kununua na kupatikana kwa bidhaa za afya ikiwemo pia athari za bei tofauti.
 
Kwa muijbu wa azimio hilo, lengo ni kusaidia nchi wanachama kuchukua uamuzi bora na sahihi wakati zinanunua bidhaa za afya, kuafikia bei nafuu na halikadhalika kufanikisha huduma za afya kwa watu wao.

WHO inasema uhakika wa kupatikana dawa ni nguzo ya kuboresha huduma za afya na pia utabainisha mwelekeo wa WHO katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Nchi wanachama zilionyesha nia yao kwa mpango wa WHO wa kuhakikisha uwepo wa dawa, chanjo na bidhaa zingine za afya.

 

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
1'13"
Photo Credit
Photo: Sean Kimmons/IRIN