23 Mei 2019
Leo katika Jarida na Habari la Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea
-Umoja wa Mataifa watangaza mikakati mipya ya kukabiliana na Ebola Congo DRC, chini ya utaribnu maalum wa David Gressely
-Huko nchini Kenya kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini familia moja yamrejesha ndoto ya masomo mkimbizi kutoka Burundi
-Chama cha wanawake cha misaada ya kisheria Côte d’Ivoire chajitosa kuwasaidia wasio na utaifa.
-Makala yetu leo ni SDGs tunabisha hodi mjini Nakuru nchini Kenya ambako tunakutana na mwanaharakati wa mazingira anayepiga vita matumizi na utupaji kiholelea wa mifuko ya plastiki
-Mashinani tunakwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ambako ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSCA umesambaza maji bila gharama yoyote kwa wakazi wa mji mkuu Bangui, na wananchi wamefunguka nyoyo zao