Mradi wa msichana mmoja baiskeli moja unafanikiwa, tunakusudia kwenda Tanzania nzima-Sara Bedah

21 Mei 2019

Umbali wa kufika shuleni ni moja ya changamoto zinazochangia kukwamisha malengo ya wasichana wengi ya elimu hususani katika nchi nyingi zinazoendelea. Kwa mujibu wa takiwmu za mashirika mbalimbali likiwemo la Umoha wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF na la elimu, sayansi na utamadubni UNESCO umbali wa kufika shuleni unachangia utoro , mimba za utotoni n ahata mafanikio duni katika masomo na hatimaye maishani kwa wasichana. Hata hivyo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali ili kuyatekeleza malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs ikiwemo lengo namba 4  la kuhakikisha elimu kwa wote pamoja na usawa wa kijinsia wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali za kusaidia kufikia lengo holo.

Mathalani nchini Tanzania mradi wa ‘Msichana mmoja, baiskeli moja’ unaoendeshwa na shirika la Msichana Initiative wa kuwapatia baiskeli wanafunzi wasichana wanaotembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 kwenda kusaka elimu, umeanza kuzaa matunda kutokana na ufaulu wa wasichana hao kuongezeka. Sara Bedah, afisa mawasiliano wa shirika la Msichana Initiative katika mahojiano haya na Arnold Kayanda anaeleza hatua ambayo wameipiga tangu walipoanza kusambaza baiskeli hizo mkoani Dodoma na Lindi.

Audio Credit:
Grace Kaneiya/ Arnold Kayanda/ Sara Bedah
Audio Duration:
4'14"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud