Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila nyuki upatikanaji wa chakula duniani mashakani- FAO

Bila nyuki upatikanaji wa chakula duniani mashakani- FAO

Pakua

Leo ni siku ya nyuki duniani siku ambayo inatanabaisha umuhimu wa nyuki na tishio linalowakabili viumbe hao, kutoweka kwao utakuwa mtihani mkubwa kwa dunia  limesema shirika la chakula na kilimo FAO  hususani kwa mustakabali wa chakula . Flora Nducha na maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa FAO asilimia 75 ya matunda na mbogamboga visingekuwepo bila nyuki na ni bidhaa ambazo ni muhimu sana kwa uhakika wa chakula na bayoanuai ya dunia .

Hata hivyo shirika hilo linasema nyuki wanakabiliwa na tishio kubwa dhidi ya wachavuaji wake zikiwemo aina zaidi ya 20,000 za nyuki, na  pia wadudu wengine na hata wanyama kama popo na nyani ambao pia wanaweza kufanya kazi ya kuchavusha.

Afisa kilimo na mtaalamu wa masuala ya uchavuaji wa FAO Abram Bicksler anasema takwimu ziko bayana na kwamba hatua zisipochukuliwa sasa kudhibiti vyanzo vya tishio hilo hali itakuwa mbaya zaidi katika siku za usoni, hasa ukizingatia baadhi ya sehemu za Amerika na ulaya idadi ya nyuki imepungua sana.

Akifafanua zaidi kuhusu vyanzo vya tishio la mustakbali wa nyuki duniani Bicksler amesema, “ni mchanganyiko wa sababu mbalimbali ambazo zote zinachangiwa na shughuli za binadamu , hivyo mabadiliko ya tabianchi ni sababu, kutopea kwa makazi ni sababu, matumizi ya kupindukia ya dawa za kuua wadudu ni sbababu kubwa lakini pia magonjwa makubwa na wadudu pia vinaathiri  wachavuaji hivyo sababu hizi vikiwekwa kwa pamoja wachavuaji wetu wanakabiliwa na wakati mgumu.”

Naye mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva akisisitiza umuhimu wa nyuki amesema. "zaidi ya asilimia 75 ya mazao ya chakula yanatememea kwa akiasi fulani uchavushaji wa nyuki na matumizi na ubora , kutokuwepo kwa nyuki na wachavushaji wengine  kutaangamiza kahawa, Alimondi, tufaa, nyanya na kokoa kwa kutaja mazao machache tu ambayo yanategemea uchavushaji.”

Amezihimiza nchi zote kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha wanalinda nyuki .Haya ni maadhimisho ya pili ya kimataifa ya siku ya nyuki duniani abaada ya kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa mwaka 2017 na kuanza kuadhimishwa rasmi Mei 20 mwaka jana.

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Flora Nducha
Sauti
2'3"
Photo Credit
FAO