20 Mei 2019

20 Mei 2019

Je wajua kuwa bila nyuki uhakika wa chakula duniani uko mashakani? Hii leo ikiwa ni siku ya nyukia duniani tunakukutanisha na wabobezi kufahamu nyuki na faida zake. Tunakwenda Sudan Kusini kuangazia jinsi Umoja wa Mataifa umetembelea jamii moja huko Lobonok kuchagiza haki za binadamu na nchini Kenya teknolojia imeleta nuru kwa mtoto mkimbizi ambaye alizaliwa bila miguu. Kwenye makala Mkurugenzi Mkuu wa shirika la hali ya hewa Tanzania, azungumzia jinsi ambavyo wanatumia teknolojia kukabili majanga na mashinani leo ni walinda amani wanawake kutoka Tanzania na harakati zao za doria za kuleta amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Mwenyeji wako ni Grace Kaneiya, karibu!

Audio Credit:
Grace Kaneiya
Audio Duration:
12'3"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud