Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uelimishaji jamii kuhusu uhifadhi endelevu wa misitu ni suala mtambuka

Uelimishaji jamii kuhusu uhifadhi endelevu wa misitu ni suala mtambuka

Pakua

Elimu kuhusu uhifadhi endelevu wa misitu ni moja ya ajenda muhimu katika harakati za Umoja wa Mataifa  za kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs au ajenda 2030. 

Nchi mbalimbali duniani kote zinahimizwa kuhamasisha jamii za mashinani kuzingatia suala la uhifadhi wa misitu ili kulinda mazingira, vyanzo vya maji na kadhalika, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa mataifa hayo ikishirikiana na wadau. Ni katika muktadha huo leo katika makala yetu, Patrick Newman wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefanya mahojiano na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest Mero pamoja na mtafiti na mwalimu kutoka Chuo Kikuu cha Eastern Finland kilichopo nchini Finland, Irmeli Mustalathi , ambapo wamezungumzia mikakati shirikishi kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo nchini Tanzania na kile cha Eastern Finland kuhusu  uelimishaji  jamii za mashinani juu ya umuhimu wa uhifadhi endelevu wa misitu katika mikoa ya kati nchini Tanzania.

Audio Credit
Patrick Newman/ Grace Kaneiya
Audio Duration
4'23"
Photo Credit
UNMISS/Eric Kanalstein