Jaridani leo tunamulika suala la usalama barabarani kwa kuzingatia hii ni wiki ya usalama barabarani. Tunaanzia nchini Uganda kuzungumza na manusura wa ajali za barabarani na kisha tunawekwenda Tanzania kuzungumza na mabalozi wa usalama barabarani na mmoja wao ni James Rock Mwakibinga. Na mamlaka za usalama barabarani nchini humo zinasemaje? Kamanda Fortunatus Muslim amefafanua hatua wanazochukua kupunguza ajali na leo Ijumaa ni neno la wiki Onni Sigalla kutoka BAKITA anafafanua maana ya mtu Mkulivu. Usisahau kuna habari kwa ufupi Priscilla Lecomte anakupatia kwa muhtasari habari muhimu, na mwenyeji wako leo ni Arnold Kayanda, karibu.