Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya kukusanya kauri ziwani ni hatari sana kwetu lakini hatuna jinsi - Wanawake ziwa Albert, Uganda.

Kazi ya kukusanya kauri ziwani ni hatari sana kwetu lakini hatuna jinsi - Wanawake ziwa Albert, Uganda.

Pakua

Ni kawaida mtu kufurahia sahani, kikombe au birika iliyotokana na ufinyazi wa udongo au kauri. Lakini je wafahamu suluba yake, hasa kwa ukusanyaji wa kauri hiyo katika nchi zinazoendelea? Hali inafahamika fika kwa wanawake wanaojishughulisha na kazi hiyo  katika ziwa Albert nchini Uganda ambao kutokana na madhila wanayopitia ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini, wameiomba serikali ya Uganda 'iwapige jeki' ili waiache kazi hiyo ngumu inayohatarisha maisha yao.

Soundcloud

Kama lilivyo lengo namba moja la maendeleo endelevu linalosaka kuondoa umaskini ifikapo  mwaka 2030, na lengo namba tatu linaongelea afya bora na ustawi wa jamii nzima, mbunge mwanamke wa wilaya ya Buliisa Norah Bigirwa Nyendwoha anahaha kuwapigania wanawake hao  waweze kuishi kwa kadri ya malengo hayo yanayofanyiwa kazi na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa ili yote 17 yawe yamefikiwa ifikapo mwaka 2030.

John Kibego amezuru kandoni mwa ziwa Albert na kutuandalia makala hii.

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
Picha: UNHCR/M. Sibiloni