Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umeme wa sola washika kasi Tanzania,  UNDP yaonyesha njia

Umeme wa sola washika kasi Tanzania,  UNDP yaonyesha njia

Pakua

Lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015, yanataka pamoja na mambo mengine kuhakikisha nishati ya kisasa iliyo nafuu na ya uhakika inapatikana ili kufanikisha shughuli za kila siku za maendeleo. Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mpango wa maendeleo, UNDP limeamua kuonyesha njia kuwa hilo linawezekana kwa kuwa kuwekeza kwenye sola mwanzoni ni gharama lakini ni gharama inayopunguza gharama za usoni. Je ni kwa vipi/ Stella Vuzo wa kituo cha  habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na meneja mradi wa kampuni ya kufunga paneli za sola Baraka Solar Specialists ambao wana jukumu wa kufunga mradi huo UNDP. Meneja mradi huyo Yuda Thadeus Asenga anasema kuwa hatimaye paneli 690  wanazofunga zitazalisha Kilowati 280 za umeme. Lakini kwa ujumla mapokeo ya huduma za sola yako vipi?

Audio Credit
Grace Kaneiya/Stella Vuzo
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
Mohamed Nasser