29 Aprili 2019

29 Aprili 2019

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Patrick Newman anakuletea 

-Jopo la Umoja wa Mataifa limetoa ripoti kuhusu usugu wa vijiumbe maradhi likisema hakuna muda wa kusubiri, usugu wa dawa ni janga la kimataifa na hatua zichukuliwe sasa

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linahitaji dola milioni 29 ili kukidhi mahitaji ya lazima kwa watoto 300,000 wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela walioko Colombia

-Teknolojia ya fedha kiganjani yasaidia wanawake kujiimarisha kibiashara huku wakitunza familia zao nchini  Kenya

- Makala yetu leo inaangazia wafugaji wa asili nchini Tanzania na juhudi wanazochukua kuhimili mabadiliko ya tabianchi

-Na mshinani utamsiki mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la Christ Daughters linalosaidia watoto wa kike mkoani Mwanza kuachana na ukahaba lakini pia kuwapa mafunzo

Audio Credit:
UN News/Patrick Newman
Audio Duration:
13'27"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud