Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je wafahamu kuna vazi linaloweza kukuepusha na Malaria ?

Je wafahamu kuna vazi linaloweza kukuepusha na Malaria ?

Pakua

Kila uchao harakati zinaendelea ili kuhakikisha kuwa ugonjwa wa Malaria uliosababisha vifo vya watu zaidi ya 400,000 mwaka 2017 unatokomezwa duniani kote. Hali ya ugonjwa  huo ni mbaya zaidi katika nchi 11 ambazo Burkina Faso, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRc, Ghana, India, Mali, Msumbiji, Niger, Nigeria, Uganda na Tanzania. Serikali, mashirika na taasisi za kiraia zinabonga bongo kuibuka na mkakati wa kuondokana na ugonjwa  huo unaozuilika ambapo mbinu ya karibuni zaidi ni ile ya kutengeneza vazi ambalo kwamo katu mbu anayeeneza ugonjwa wa Malaria hawezi kusogea. Je ni kwa vipi basi? Na ni nani huyo? Patrick Newman anakufafanulia kwa kina.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Patrick Newman
Audio Duration
4'13"
Photo Credit
Picha na UNICEF/UNO72220/Phelps