Harakati za wanawake kusaka sauti katika Kaunti ya Kisii nchini Kenya.
Umoja wa Mataifa na mashirika yake kwa pamoja wamekuwa mstari wa mbele kupigia chepuo suala la usawa kijinsia katika kila jamii hususan katika nafasi ya uongozi ili kuhakikisha mwanamke anapewa nafasi katika maendeleo ya jamii yake.
Nchini Kenya kama ilivyo pia katika mataifa mengine duniani, juhudi za kumwinua mwanamke zinaendelea japokuwa katika baadhi ya maeneo bado nafasi ya mwanamke inazidi kukandamizwa katika nyanja ya maamuzi hivyo kupelekea ajenda ya kumkomboa mwanamke kutopewa kipaumbele katika miswada mbalimbali bungeni.
Flora Nducha wa Idhaa ya kiswahili alipata fursa na kuzungumza na Bi Karen Magala ambaye ni mwenyekiti wa wanawake katika bunge la kaunti ya Kisii nchini Kenya . Katika mahojiano yao kandoni mwa mkutano wa hali ya wanawake CSW63 jijini New York, Bi Magala anaanza kwa kueleza changamoto wanazokabiliana nazo.