Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nguva warejea Madagascar, ni baada ya wananchi kuchukua hatua

Nguva warejea Madagascar, ni baada ya wananchi kuchukua hatua

Pakua

Uharibifu wa mazingira unazidi kutishia siyo tu uhai wa binadamu bali pia viumbe vingine vinavyoishi nchi kavu na hata baharini. Miongoni mwa viumbe vilivyo hatarini ni nguva ambao uwepo wao baharini unasaidia kumea kwa mimea ya baharini iliyo muhimu kwa chakula cha samaki. Ni kwa kuzingatia hilo Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linatilia mkazi uhai wa viumbe vilivyo chini ya maji, ikiwemo baharini. Nchini Madagascar, kuongezeka kwa idadi ya watu kunatia shinikizo kwenye mazingira na nguva wako hatarini. Hata hivyo jamii zinazozunguka fukwe kwa kutambua umuhimu wa nguva hao na viumbe vingine, wamechukua hatua, je ni zipi? Grace Kaneiya anakuletea kwa kina.

Audio Duration
3'50"
Photo Credit
UN