Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, leo ameukumbusha uongozi wa Sudan kuhusu wajibu wake kimataifa wa kuhakikisha unalinda haki za binadamu kwa watu wote na kujizuia na machafuko.
Majaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC hii leo kwa kauli moja wametupilia mbali ombi la mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Fatou Bensouda ya kutaka kufanya uchunguzi dhidi ya kile kinachodaiwa kuwa ni vitendo vya uhalifu wa kivita na kibinadamu vilivyofanyika nchini Afghanistan.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka vijana kote duniani kushika hatamu za kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s kwa sababu sauti zao ni muhimu na uwezo wanao.
Na katika mada kwa kina, mjadala unahusu umuhimu wa bima ya afya kwa wote.