Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kunusuru kaya maskini Tanzania ni chachu ya kufanikisha SDGs- Tumpe

Mpango wa kunusuru kaya maskini Tanzania ni chachu ya kufanikisha SDGs- Tumpe

Pakua

Katika jitihada za kufanikisha lengo namba moja la malengo 17 ya maendeleo endelevu,SDGs, la kutokomeza umaskini,  Tanzania ilianzisha mfuko wa maendeleo ya jamii uitwao TASAF ukiwa na lengo la kuzinusuru kaya maskini zaidi.

Tumpe Mnyawami Lukongo ni mtafiti , mchambuzi na mtaalamu kutoka mfuko huo wa TASAF, katika  mahojiano haya na Assumpta Massoi kandoni mwa mkutano wa kutathimini hali ya wanawake duniani CSW63 uliofanyika New York Marekani, anaeleza mafanikio ya mfuko huo na namna unavyowafikia walengwa.

Tumpe Mnyawami Lukongo anasema mpango wa TASAF umezifikia kaya milioni moja na laki  moja na katika utekelezaji wake, mradi ulizingatia usawa wa kijinsia hasa katika suala zima la kuinua uchumi wa mwanamke, “hii ilitokana na majaribio yaliyofanywa katika wilaya tatu kabla ya huo mpango ambapo ilionekna fedha zikipokelewa na wanaume, baadhi yao wanazitumia katika mambo ambayo hayako katika malengo ya mpango lakini mama akipokea hasa mama anayetoka katika kaya maskini, kaya nzima, kwa kuhusisha hata baba, utakuta ile hela inamsaidia.”

Bi Lukongo anaeleza kuwa kiwango cha fedha wanachopewa wanachopewa kaya maskini kinatofautiana kulingana na uhitaji lakini zaidi ni kwamba kila kaya inayotambuliwa kuwa ni maskini, inapata kiwango sawa na kaya nyingine yoyote maskini isipokuwa kiasi kinaongezeka pale ambapo kuna vigezo vya ziada kama idadi ya wanafamilia na uhitaji wa ziada kama vile kaya kuwa na watoto walioko katika masomo au mahitaji ya afya.

“Kiwango cha juu kabisa ni 38,000 kwa mwezi na tunalipa miezi miwili kwa mkupuo ili kuepuka zile gharama za kuzipeleka zile hela kwa walengwa.” Anasema mtaalamu Tumpe Mnyawami Lukongo.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'32"
Photo Credit
UNEP-UNDP Rwanda/ Jan Rijpma