Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wa kabila la Endorois wachukua hatua kulinda lugha yao

Vijana wa kabila la Endorois wachukua hatua kulinda lugha yao

Pakua

Lugha ni utambulisho muhimu katika jamii ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, baadhi ya lugha ziko hatarini kutoweka. 

UNESCO inataja lugha kuwa hatarini kutoweka iwapo wenyeji wa lugha wanaacha kuitumia kabisa au wanatumia mara chache tu kuwasiliana na pale lugha haipitishwi kutoka kizazi kimoja au kingine. Aidha hakuna mtu mzima au mtoto anayezungumza lugha hiyo. Moja ya lugha ambazo ziko hatarini kutoweka ni ile  ya jamii ya Endorois kutoka Kenya ambapo sasa vijana wamechukua hatua kuilinda. Katika kufahamu hatua hizo, Grace Kaneiya wa Idhaa hii ya kiswahili amezungumza na Carson Kiburo Kibet wa jamii ya asili ya Endorois kutoka mtandao wa vijana wa asili kimataifa ambaye ameshiriki jukwaa la vijana hapa New York, Marekani  lililofunga pazia Jumanne wiki hii ambaye anaelezea juhudi za kulinda sio tu lugha yake lakini pia utamaduni wa jamii yake. 

Audio Credit
Arnold Kayanda/Grace Kaneiya/
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
UN/Patrick Newman