Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tunawaandaa ili waepukane na vishawishi potofu- KKKT

Vijana tunawaandaa ili waepukane na vishawishi potofu- KKKT

Pakua

Matizo la uhamiaji ni moja ya changamoto kubwa katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 umesema mkutano wa 52 wa Umoja wa Mataifa wa Kamisheni ya idadi ya watu na maendeleo CPD ambao unafunga pazia hii leo. 

Mkutano huo ulioleta washiriki zaidi ya 125 wakiwemo mawaziri 60, umezitaka nchi wanachama kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha vijana wanapata fursa stahiki na vitu vitakavyowashawishi kutofunga safari za hatari kwenda ughaibuni kusaka mustakhbali bora.

Miongoni mwa washiriki katika mkutano huo ni Dkt. Paul Zebadia Mbano, mkurugenzi wa programu za afya wa KKT Tanzania (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anafafanua sababu za vijana hao kufungasha virago.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
6'7"
Photo Credit
Mwanza Youth reporter