Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utoaji taarifa na vyombo vya habari muhimu katika kuhakikisha ulinzi wa wasichana na wanawake-IPPFA

Utoaji taarifa na vyombo vya habari muhimu katika kuhakikisha ulinzi wa wasichana na wanawake-IPPFA

Pakua

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba asilimia 78 ya wanawake walio ndani ya ndoa au wanaoishi katika mazingira ya ndoa wanaweza kupata huduma za mpango wa uzazi, hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 72 tangu mwaka 1994, lakini idadi hiyo inapungua hadi chini ya asilimia 50 katika mataifa 44, mengi yakiwa Afrika  kusini mwa jangwa la Sahara na mataifa ya kusini mwa visiwa vya pacific.

Kwa kuzingatia hali hii halisi mashinani sasa mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali yamechukua hatua kufanya kazi na jamii hususan wanawake na wasichana katika kukabiliana na changamoto zinazokabili kundi hilo ikiwemo, ukatili wa kijinsia, maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi, ndoa za utotoni na ukeketaji. Moja ya mashirika hayo ni International Planned Parenthood Federation Africa, IPPFA linalojihusisha na afya ya uzazi ambapo mshauri wa uelimishaji Emma Bawo katika mahojiano maalum na Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano wa 52 wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo, CPD ameelezea wanachofanya ili kuhakikisha afya ya mwanamke

(Sauti ya Emma)

Bi. Bawo amekwenda mbali zaidi na kutaja changamoto za ulinzi wa wanawake na wasichana

(Sauti ya Emma)

Mkutano wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo unafanyika hapa New York Marekani na utakamilika Aprili 5.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
2'25"
Photo Credit
UN/Eskinder Debebe