Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhifadhi wa misitu unahitaji ushiriki wa jamii, serikali na mashirika- FAO Kenya

Uhifadhi wa misitu unahitaji ushiriki wa jamii, serikali na mashirika- FAO Kenya

Pakua

Misitu na miti kwa ujumla vina faida na mchango mkubwa kwa ajili ya maisha ya watu lakini pia sayari Dunia, kuimarisha vipato, kuleta hewa safi, kuwa ni vyanzo vya maji, ulinzi wa bayoanuai na hata kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO misitu ina changia kwa kiasi kikubwa  kama chanzo cha chakula na hata dawa na isitoshe misitu ni moja ya mihimili ya maendelea ya kijamii na kiuchumi na hususan kwa mamilioni ya watu vijijini ikiwemo katika mataifa maskini. Licha ya kwamba misitu ni uhai ,uhifadhi wakeunakabiliwa na changamoto mbali mbali kama anavyosema Gabriel Rugalema, mwakilishi mkazi wa FAO, Kenya. Katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa hii anaanza kwa kufafanua matumizi ya misitu.

Audio Credit
Flora Nducha/ Grace Kaneiya/ Gabriel Rugalema
Sauti
3'53"
Photo Credit
UNMISS/Eric Kanalstein