Jaridani Machi 22, 2019 na Grace Kaneiya
-Habari kwa ufupi zimeangazia siku ya maji duniani ambayo huadhimishwa kila mwakla Machi 22 ambapo Tanzania imeelezea mipango ya kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma ifikapo mwaka 2030, Pia mashirika ya kibinadamu yanahaha kusadia waathirika wa kimbunga Idai na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP laonyesha pengo kubwa kati ya nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea.
Mada kwa kina imeangazia kamisheni ya hali ya wanawake CSW63 hususan Kenya na harakati za wanawake kuchagiza amani nchini mwao.
Neno la wiki linachambuliwa neno Hidaya