Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea
-Siku ya kutokomeza ubaguzi wa rangi duniani wito umetolewa na UN kukomesha aina zote za itikadi na misimamo ya chuki vilevile ubaguzi wa kisiasa na kijamii
-Hata kama wanamatatizo ya uwezo wa kujifunza au down Syndrome watoto wote wanapaswa kutoachwa nyuma kielemu , Uganda yachukua hatua kuhakikisha hawaachwi.
-Elimu kuhusu utunzanzi na uhifadhi wa misitu ni muhimu kwa maendeleo endelevu limesema shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO
-Makala leo inaangazia utamaduni unaokwamisha amendeleo ya mwanamke na msichana mkoani Pwani nchini Tanzania
-Na mashinani tuko kwenye mkutano wa CSW63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani ukuhusu mbinu za kukabiliana na kutokuwepo usawa wa kijinsia