Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku tatu za maombolezo zaanza Msumbiji huku CERF ikitoa dola milioni 20 kusaidia katika mafuriko: OCHA

Siku tatu za maombolezo zaanza Msumbiji huku CERF ikitoa dola milioni 20 kusaidia katika mafuriko: OCHA

Pakua

Watu zaidi ya 500 wamepoteza maisha Zimbabwe, Malawi na Msumbiji kutokana na mafuriko yaliyosabnabishwa na kimbuga IDAI na kuwaacha maelfu bila makazi wakihitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Leo mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa  umetangaza dola milioni 20  kusaidia waathirika.

Kwa mujibu wa mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Mark Lowcock mfuko huo wa dharura CERF umetangaza kutenga dola miloni 20 kwa ajili ya kupiga jeki msaada wa kibinadamu kufuatia kimbunga Idai kilichokumba nchi tatu ikiwemo Msumbiji, Zimbabwe na Malawi huku kipaumblele ikitolewa kwa Msumbiji iliyoathirika zaidi na ambayo imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Machi 20 ili kuzika waliopoteza maisha.

Kupitia taarifa ya OCHA, bwana Lowcock amesema fedha hizo zitatumika kuimarisha juhudi za mamlaka ya nchi hizo tatu ikiwemo kwa kutoa huduma ya afya, usalama wa chakula, ulinzi, lishe bora na elimu .

Aidha mkuu huyo wa OCHA amesema makundi ya watu walio hatarini ikiwemo watoto, wanawake wajawazito na wanaonyonysha, watu wanoishi na ulemavu na walio na magonjwa ya muda mrefu ndio watakaopewa kipaumbele.

OCHA imesema fedha hizo pia zitasaidia mashirika ya kibinadmu kuimarisha mipango yao ikiwemo mbinu za kuwasiliana na kuimarisha huduma za maji na huduma za dharura za afya jwa ajili ya kupunguza hatari ya magonjwa yanayoambukizwa kupitia maji na viini.

Bwana Lowcock hatahivyo amesema mgao huo kutoka kwa CERF ni wa kukabiliana na dharura za hivi sasa lakini hautoshi kuweza kukabiliana na mahitaji ambayo yanatarajiwa kuimarika na hiyvo ametoa wito kwa wafadhili kuchangia fedha kwa ajili ya watu walioathirka kufuatia kupigazkwa kimbunga Idai.

Kimbunga Idai kilipiga mji wa Beira katika jimbo la Sofala katikati mwa Msumbiji usiku wa Machi 14 na 15 ambapo kabla ya hapo kulishuhudiwa mvua kubwa na mafuriko katika nchi tatu ikiwemo Msumbiji, Zimbabwe na Malawi na kusababisha maelfu ya watu kufurushwa makwao na vifo na uharibifu wa mali.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
2'22"
Photo Credit
WFP/Maktaba