Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake kutokuwa na sauti kunachochea ndoa za utotoni na ukeketaji Kajiado, Kenya- Bi. Parit

Wanawake kutokuwa na sauti kunachochea ndoa za utotoni na ukeketaji Kajiado, Kenya- Bi. Parit

Pakua

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake kikao cha 63 unaendelea hapa New York, Marekani ambapo vikao mbali mbali vinafanyika katika kupaza sauti za wanawake na kujadili changamoto wanazokabiliana nazo lakini pia jinsi ya kuzitatua.

Suala la ndoa za utotoni ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazozikabili jamii nyingi  na huku Umoja wa Mataifa usisitiza tatizo hilo lililomea mizizi na kuwa kama donda ndungu lazima likomeshwe kabla yam waka 2030. Hivi sasa jserikali, jamii n ahata wanaharakati wameamua kulivalia njuga suala hilo . Mmoja wa wanaharakati hao ni mwanamke Dorcus Parit mwanzilishi na mkurugenzi wa  kituo cha mpito cha Hope Beyond huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambacho ni kimbilio kwa wasichana wanaoingizwa kwenye ndoa za utotoni au wale wanaokabiliwa na hatari ya kukeketwa.  

Kandoni mwa mkutano huo wa CSW63 Bi Parit amesema idadi ya wasichana wanaokabiliwa na hali hii ni wengi huku akitoa mfano.

(Sauti ya Parit)

Halikadhalika amelalamikia kwamba bado wanawake wanakandamizwa na hivyo

(Sauti ya Parit)

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
2'2"
Photo Credit
UN Women/Ryan Brown