Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunalinda amani lakini pia twawajengea uwezo wa kujipatia kipato- Mlinda amani wa Tanzania nchini DRC

Tunalinda amani lakini pia twawajengea uwezo wa kujipatia kipato- Mlinda amani wa Tanzania nchini DRC

Pakua

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO wamezungumzia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wanayowapatia wanawake nchini humo yamebadili maisha yao.

Miongoni mwa walinda amani hao ni Kapteni Mercy Kayonde aliyepo eneo la Masizi, huko Beni jimbo la Kivu Kaskazini ambaye katika mahojiano kwa njia ya simu na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefafanua kwa kina kile wanachofanya..

Audio Credit
Grace Kaneiya/Assumpta Massoi
Audio Duration
2'6"
Photo Credit
MONUSCO