Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MSF na ALIMA wafunga virago Katwa na Butembo, ni baada ya vituo vyao vya kutibu Ebola kushambuliwa

MSF na ALIMA wafunga virago Katwa na Butembo, ni baada ya vituo vyao vya kutibu Ebola kushambuliwa

Pakua

Kufuatia matukio ya kutiwa moto kwa kituo cha kutibu Ebola cha Katwa na kile cha Butembo kushambuliwa na watu wasio na silaha wasiojulikana, vyote jimboni Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeripotiwa hii leo kuwa vituo hivyo viwili sasa havifanyi kazi kabisa. Shirika la afya ulimwenguni, WHO ambalo limelaani kitendo hicho, sasa linahofu kuwa ugonjwa huo unaweza kusambaa zaidi kutokana na hatua ya baadhi ya mashirika ya kiraia kuondoa wafanyakazi wake kutoka eneo hilo. Martial Papy Mukeba wa Radio  Okapi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO anaripoti zaidi.

 

Audio Credit
flora Nducha/Martial Papy Mukeba
Audio Duration
1'59"
Photo Credit
UNICEF/Guy Hubbard