Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko madaktari walinda amani mmenifanyia jambo la ajabu- Mzee mkazi wa MOPTI, Mali

Heko madaktari walinda amani mmenifanyia jambo la ajabu- Mzee mkazi wa MOPTI, Mali

Pakua

Nchini Mali operesheni FADEN-6 ya ujumbe wa Umoja wa  Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSMA umeleta matumaini kwa jamii hususan zile ambazo hazikuwa na matumaini ya kupata siyo tu matibabu bali pia maridhiano baina yao. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

Operesheni FADEN 6 hujumuisha shughuli za kijeshi na kiraia ikiwemo huduma bure za tiba, uhamasishaji wa masuala ya elimu na utangamano wa kijamii sambamba na haki za binadamu na usambazaji wa vifaa kwa jamii.

Hii leo kwenye kwenye eneo la Koro, jimbo la Mopti nchini Mali mpakani na Burkina Faso walinda amani wa Umoja wa Mataifa chini ya operesheni hiyo wanaonekana wakiendesha doria kwenye eneo hili ambalo kumekuwepo na mapigano kati ya wakulima na wafugaji.

Mwaka 2018 mapigano kati ya pande mbili hizo yalisababisha vifo  hali ambayo imesababisha MINUSMA kuandaa kikao cha maridhiano, huko Yorou na Koro sehemu ya utekelezaji wa azimio namba 2423 la mwaka 2018 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wakazi wa Koro na Yorou walijitokeza kushiriki mazungumzo hayo kwa lengo la kumaliza chuki kati  yao, ambapo awali wakazi wa Yorou hawakuweza kufika Koro, halikadhalika wa Koro hawakuweza kufika Yoro.

Hata hivyo baada ya maridhiano kuna mabadiliko na Abdramane Sayi, mkuu wa kijiji cha Dangatene mjini Koro ni shuhuda.

“Hii leo kutokana na juhudi zenu, naeza kwenda Yorou, na wao wanaweza kufika hapa kwetu. Wajumbe wa Kamati ya maridhiano wanaweza kufika hapa bila shida yoyote.”

Pamoja na kusaidia maridhiano, walinda amani hawa kutoka Senegal wanasaidia kutoa huduma za afya. Kouny Werme amepatiwa matibabu..

« Madaktari hawa vijana wameniwekea kitu kwenye macho yangu na imefanya nijisikie vizuri na matokeo yamekuwa ya haraka. Asante Mungu. »

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
1'49"
Photo Credit
UN Photo/Marco Dormino