Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gereza jipya Somalia kusaidia kuimarisha amani

Gereza jipya Somalia kusaidia kuimarisha amani

Pakua

Gereza lililojengwa mjini Mogadishu nchini Somalia kwa ubia kati ya Umoja wa Mataifa na wadau wake, litasaidia katika siyo tu harakati za kukabiliana na ugaidi bali pia utawala bora.

Uzinduzi wa gereza hilo lililoanza kujengwa mwezi Disemba mwaka 2015  umefanywa na Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire na ni moja ya miradi mikubwa ambayo imetekelezwa katika awamu tatu na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambamba na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC na ofisi ya miradi ya Umoja wa Mataifa, UNOPS kwa udhamini wa serikali ya Denmark, Uholanzi na Uingereza.

Ni jengo hilo ambalo linaipa mahakama nchini humo miundombinu muhimu ya kutekeleza majukumu yake katika mazingira salama kwa ajili ya wafanyakazi wa mahakama na magereza pamoja na watuhumiwa.

Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire amesema,

“Ni matumaini yangu kuwa jengo hili litawahudumia wale ambao wamepotoshwa na itawapunguzia kazi maafisa wa sheria na pia wale wanaofanya kazi katika sekta ya kurekebisha tabia”  

Hatua ya kwanza ya mradi imekamilika ikiwa na chumba cha mahakama, gereza lenye ulinzi mkali likiwa na vitanda 250, makazi ya majaji, waendesha mashitaka na wanasheria wakati wa kesi. Hatua inayofuata itaongeza vyumba zaidi vya gereza na mahakama.

Kwa upande wake, mwakilishi wa  kanda wa UNODC,  Amado De Andres amesema,

“Bila amani, utulivu na taasisi thabiti, zinazowajibika na zinazozingatia utawala wa sheria, hatuwezi kuwa na tumaini la maendeleo endelevu na halisi kwa wote”

Ili kuwa na jengo ambalo linazingatia sheria za viwangio vya Umoja wa Mataifa vya wafungwa, UNODC pia toa msaada wa wa kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa mahakama ili kuhakikisha hukumu zinakuwa za haki.

Audio Credit
Amina Hassan
Audio Duration
1'53"
Photo Credit
OCHA/Cecilia Attefors