Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana mwanafunzi  Tanzania aanzisha klabu kuwasaidia wanafunzi wasioona wafurahie haki ya elimu 

Kijana mwanafunzi  Tanzania aanzisha klabu kuwasaidia wanafunzi wasioona wafurahie haki ya elimu 

Pakua

Leo Februari 20 ni siku ya kimataifa ya haki za kijamii ikibeba kauli mbiu, ukitaka amani na maendeleo fanyia kazi haki za kijamii. Umoja wa Mataifa umesema haki hizi ni muhimu kwa ajili ya kuishi kwa amani na maendeleo. Haki za kijamii zinaendelezwa pale vikwazo ambavyo watu wanakumbana navyo kwa misingi ya jinsia yao, umri, rangi, dini , utamaduni au kuishi na ulemavu. Halikadhalika unasisitiza kuwa haki za kijamii ni kiini cha lengo katika kuimarisha maendeleo na utu.  Wito huo umeitikiwa na kijana Paul Mwame Sauli akiwa nchini Tanzania ambaye licha ya ujana wake ametambua umuhimu wa elimu jumuishi na hivyo kuchukua hatua kuziba pengo katika upatikanaji wa elimu jumuishi kwa wote ikiwemo watu wanaoishi na ulemavu. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii ambapo kijana Paul anaanza kwa kujitambulisha.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Grace Kaneiya
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
© UNICEF/Pirozzi