Katika jarida letu la Habari kwa kina ijumaa ya leo Arnold Kayanda anazungumza na mtayarishaji wa maonesho ya sanaa za asili kutoka barani afrika , Mtanzania Rose Luangisa ambaye hivi karibuni ameshiriki maonesho ya Umoja wa Mataika yaliyofanyika makao Makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani yakiwa na kaulimbiu "sanaa kwa ajili ya amani".
Na kama ada ya kila Ijumaa tunajifunza Kiswahili, leo hii tuko nchini Uganda kwake Aida Mutenyo, mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki anachambua maana ya neno "Afugaye ng’ombe tume, mwenye maziwa la kujaza”
-Pia tunasoma maoni yako msikilizaji uliyotuandikia kupitia ukurasa wetu wa Facebook.