Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumalizika kwa safari ya Flip Flopi sio mwisho wa uhamasishaji kuhusu plastiki:UNEP

Kumalizika kwa safari ya Flip Flopi sio mwisho wa uhamasishaji kuhusu plastiki:UNEP

Pakua

Dau la FlipFlopi lililojengwa na Ali Skanda kwa tani elfu 10 za taka za plastiki wiki iliyopita lilihitimisha ziara yake ya kuelimisha jamii kuhusu athari za taka za plastiki kwa siku 14. Ziara hiyo iliyoanza tarehe 24 mwezi Januari huko Lamu, nchini Kenya na kupitia Kipini, Malindi,Watamu, Kilifi, Mombasa, Diani, Shimoni, Wete, Pemba Kusini, Nungwi ilikamilika  tarehe 7 Februari katika Mji Mkongwe Zanzibar kwa mafanikio makubwa na kutimiza lengo lililokusudiwa. Lakini je kumaliza kwa safari hiyo ndio mwisho wa kupiga debe dhidi ya matumizi ya plastiki? Flora Nducha amezengumza na mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazinfira UNEP waandaaji wakubwa wa safari ya Dau hilo kupata ufafanuzi. Bi Clara Makenya anaanza kwa kuelezea mafanikio yao.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/Flora Nducha/Clara Makenya
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
UN Environment