Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chukua hatua sasa kutokomeza FGM ifikapo 2030:UN

Chukua hatua sasa kutokomeza FGM ifikapo 2030:UN

Pakua

Wakati wa kuchukua hatua ili kutokomeza ukeketaji  au FGM, ifikapo mwaka 2030 ni sasa . Wito huo wa pamoja umetolewa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji na wakuu  wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu UNFPA, Dkt. Natalia Kanem, lakuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore na la linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women , Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Wakitolea mfano wa athari za miala hiyo potofu watuu hao wamesema "Mary Oloiparuni alikuwa na umri wa miaka 13 tu alipolazimika kupitia kisu cha ngariba kwa uchungu mkali na kutokwa damu kupita kiasi na uchungu umeendelea hadi leo miaka 19 baadaye ambapo kila alipojifungua watoto wake watano maumivu yake hayasemeki.”

Na Mary hayuko peke yake, kwa mujibu wa tarifa hiyo ya pamoja takriban wasichana na wanawake milioni 200 walio hai hii leo wamekeketwa na kuwa waathirika wa moja ya ukatili mkubwa kabisa wa kijinsia duniani.

Juhudi zinazohitajika

Katika maadhimisho ya leo viongozi hao wamesisitiza dhamira yao ya kukomesha ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu ili mamilioni ya wasichana ambao bado wako hatarini kukeketwa ifikapo 2030 kutopitia machungu aliyopitia Mary.

“Juhudi hizi ni muhimu kwa sababu ukeketaji una athari za muda mrefu za kimwili, kisaikolojia na kijamii.Unakiuka haki za wanawake za kujamihiana na afya ya uzazi, utu wao, kutobaguliwa na uuhuru dhidi ya ukatili au kudharaulika.Pia ukeketaji unakiuka kanuni za kitabibu, na sio salama bila kujali nanani anaufanya au mazingira ni masafi kiasi gani.”

Wameongeza kuwa kwa kuwa FGM ni aina mojawapo ya ukatili hauwezi kushughulikiwa bila kujumisha mifumo mingine ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kama ndoa za utotoni. Wakihimiza kwamba ili kukomesha FGM ni lazima kushughulikia mizizi ya kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia na kuuhakikisha uwezeshaji wa wanawake kijamii na kiuchumi.

Hatua za kuchukua

Mwaka 2015 viongozi wa dunia kwa pamoja waliunga mkono utokomezaji wa FGM ifikapo mwaka 2030 kupitia ajenda ya maendeleo endelevu SDGs. Umoja wa Mataifa unasema hili ni lengo linalowezekana n ani lazima tuchukue hatua sasa kugeuza utashi wa kisiasa kuwa hatua. Viongozi hao wa Umoja wa Mataifa wakizitaja hatua hizo wamesema “Katika ngazi ya taifa tunahitaji será mpya na sheria za kulinda haki za wasichana na wanawake ili waishi huru bila ukatili na ubaguzi na kwa nchi ambazo FGM bado inaendelkea kuwe na mipango ya serikali kukomesha vitendo hivyo na mipango ijumuishe bajeti kwa ajili ya elimu, afya ya uzazi, huduma za jamii na msaada wa kisheria.”

"Katika ngazi ya kikanda, tunahitaji taasisi na jamii kufanya kazi pamoja kuzuia kitendo cha wanwake na wasichana kuvuka mipaka kwa lengo la kuwapeleka kwenye maeneo ambayo sheria kuhusu ukeketaji si kali sana ili wakafanyiwe ukatili huo.”

 Katika ngazi ya jamii tunataka viongozi wa dini kukemea dhana kwamba FGM msingi wake ni dini. Kwa sababu shinikizo la kijamii mara nyingi huchagiza vitendo hivyo, hivyo watu na familia zinahitaji kuelimishwa kuhusu faida za kuachana na mila hizo potofu.

Mchango wa jamii katika kutokomeza FGM

Viongozi hao wanasema ahadi za umma kutokomeza FGM na hususan za jamii nzima ni njia bora na ni mbinu inayofanya kazi kama jukumu la pamoja. Hata hivyo wamesema ahadi ya jamii lazima iende sanjari na mikakati ya kukosoa mila, vitendo na hulka ambazo zinakumbatia ukeketaji.

Pia wamesema simulizi za waathirika manusura kama Mary zinasaidia kujenga uelewa na uhalisia wa athari za muda mrefu za vitendo hivyo kwa Maisha ya wanawake.

Vitu vingine vinavyoweza kusaidia ni kampeni na matumizi ya mitandao ya kijamii katika kufikisha ujumbe kwamba kukomesha ukeketaji kunaboresha na kuokoa Maisha.

Wamezishukuru serikali, asasi za kiraia, jamii na watu binafsi kwa juhudi zao kwani ukeketaji unapungua, hata hivyo wamesema lengo sio kuupunguza bali ni kuutokomeza kabisa ifikapo 2030.

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
2'29"
Photo Credit
UNICEF/Samuel Leadismo