Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saratani imegusa karibu kila familia duniani- WHO

Saratani imegusa karibu kila familia duniani- WHO

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya saratani duniani, shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema kuwa kwa sasa ugonjwa huo haupaswi kuwa hukumu ya kifo kwa kuwa asilimia 50 ya aina zote za saratani inaweza kuzuilika. Arnold Kayanda na taarifa zaidi.

WHO inasema saratani takribani kila familia duniani  hivi sasa imeguswa na ugonjwa huo ambao ni chanzo cha kifo kimoja katika kila vifo sita duniani.

Ingawa hivyo shirika hilo kupitia Mkurugenzi wake wa usimamizi wa magonjwa yasiyoambukiza, Dkt. Etienne Krug, linasema mzigo wa saratani unaweza kupunguzwa kwa kutokana na uwepo wa mifumo na mbinu za kubaini na kuzuia.

“Tunafahamu visababishi vikuu vya saratani hivyo tuimarishe mifumo ya afya ili kurahisisha utambuzi na tiba ili kuokoa maisha ya mamilioni,” amesema Dkt. Krug.

Katika kuimarisha tiba na utambuzi, WHO imetoa mwongozo kwa ajili ya kukabiliana na maumivu makali yanayopata wagonjwa wa saratani.

Mwongozo huo umegawanyika katika maeneo matatu muhimu ambayo ni :mosi kushughulikia chaguo la dawa za kutumia tangu awali kudhibiti maumivu ya saratani, jinsi ya kutoa dawa hizo ikiwemo matumizi ya afyuni na wakati wa kusitisha.

Pili matumizi ya dawa mbadala kama steroids, dawa za kuondoa msongo wa mawazo na nyinginezo na tatu kudhibiti mauavu yanayohusiana na saratani ya mifupa yakijumuisha matumizi ya dawa za kuzuia kulainika kwa mifupa na matumizi ya mionzi.

Audio Credit
Flora Nducha/Arnold Kayanda
Audio Duration
1'21"
Photo Credit
PAHO