25 Januari 2019

25 Januari 2019

Jaridani hii leo Arnold Kayanda azungumza na Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wakimbizi duniani, WRC, ni baada ya kuzindua ripoti yao jijini New York, Marekani. Tunabisha hodi Geneva Uswisi ambako huko sauti imepazwa kwa mamlaka za Malawi ziache ghasia za kisiasa na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wakati huu ambapo  nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi baadaye mwaka huu. Huko Msumbiji nako mwanahabari bado anashikiliwa kwa sababu tu ya kuhoji watu waliokimbia mashambulizi. Jarida la kina hii leo ni dau la plastiki kutoka Lamu hadi Mji Mkongwe na tumezungumza na mjenzi wake. Neno la wiki ni Bughudha na uchambuzi kutoka BAKITA. Karibu!

Audio Credit:
Arnold Kayanda
Audio Duration:
10'41"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud