Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustakabali bora wa ajira uzingatie maslahi ya binadamu na si vinginevyo- Ripoti

Mustakabali bora wa ajira uzingatie maslahi ya binadamu na si vinginevyo- Ripoti

Pakua

Kamisheni ya kimataifa ya shirika la kazi duniani, ILO kuhusu mustakabali wa ajira duniani leo imesihi serikali kuweka mikakati kwa lengo la kushughulikia changamoto zinazotokana na mabadiliko makubwa katika sekta ya ajira ili hatimaye ajira siyo tu iwe ni ya utu bali pia iwe endelevu.  .

Video hii mahsusi iliyotolewa leo sambamba na uzinduzi wa ripoti ya kamisheni kuhusu mustakbali wa ajira duniani.

Ikiwa na wajumbe 27, wametoa wito huo kwa serikali baada ya uchunguzi wa miezi 15,  ikichambua changamoto za ajira ziletwazo na teknolojia mpya, mabadiliko ya tabianchi na mabadiliko ya mwenendo wa makundi ya watu duniani.

Katika video hii wakiwemo wenyeviti wenza Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na Waziri Mkuu wa Sweden Stefan Löfven, wanapendekeza dira ambamo kwayo binadamu ni kitovu cha uwekezaji wa uwezeshaji binadamu, kazi za taasisi, ajira endelevu na yenye utu.

Mathalani Rais Ramaphosa anasema “ripoti hii imekuja wakati muafaka kushughulikia changamoto ambazo zinakabili wafanyakazi wengi.”

Wanasema pia ajira ambayo inalinda haki za msingi za mfanyakazi kwa upande wa ujira unaomwezesha kuishi, saa za kazi zenye ukomo na mazingira safi na salama kwenye kazi.

Halikadhalika hakikisho la hifadhi ya jamii tangu mtu anapozaliwa hadi uzeeni, mafao ambayo yanamwezesha kukimu mahitaji yake, fursa ya kujiendeleza na kuboresha stadi zake.

Kamisheni pia inataka usimamizi bora wa mabadiliko ya teknolojia ili yawezesha kuchagiza ajira yenye utu na yasiyoengua wengine.

Wajumbe wanasema “fursa lukuki zinasubiri iwapo watu wataboresha mazingira ya kazi na kuziba pengo la jinsia kwenye ajira. Lakini hii  haiwezi kujileta bila kuamua. Bila uamuzi wa dhati tutakuwa tunaota ndota kwenye dunia ambayo pengo la ukosefu wa usawa na ukosefu wa uhakika wa maisha linazidi kuwa kubwa.”Uzinduzi wa ripoti hiyo ni sehemu ya mwanzo wa maadhimisho ya shirika la kazi duniani, ILO kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ambapo shirika linatathmini kile kilichofanyika na mwelekeo wa baadaye.

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
1'48"
Photo Credit
ILO