Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 wauawa kwenye ghasia Sudan, vikosi vya serikali vyasaka waandamanaji hadi hospitalini

24 wauawa kwenye ghasia Sudan, vikosi vya serikali vyasaka waandamanaji hadi hospitalini

Pakua

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya ghasia zinazoendela nchini Sudan ambazo hadi sasa zimesababisha kuuawa kwa watu 24 na wengine wengi wamejeruhiwa. Arnold Kayanda na ripoti kamili.

Ghasia hizo zinatokana na maandamano yaliyoanza tarehe 16 mwezi uliopita kwenye miji 14 nchini Sudan ambapo waandamanaji wanapinga ongezeko la bei za bidhaa.

Akihojiwa mjini Geneva, Uswisi hii leo, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Ravina Shamdasani amesema..

“Vikosi vya usalama wanafuata waandamanaji hadi hospitali ya Omdurman na kufyatua risasi pamoja na mabomu ya kutoa machozi. Hii kwa uhakika haikubaliki, tunatoa wito kwa mamlaka zihakikishe kuwa haki ya watu kukusanyika na kuandamana kwa amani inalindwa bila kujali mirengo yao ya kisiasa.”

Msemaji huyo amemnukuu Kamishna Bachelet akisema kuwa.

Kuna malalamiko ya kweli lakini si kwamba tunasema ni rahisi kupatia majibu. Lakini jawabu kandamizi linaweza kufanya malalamiko hayo kuwa mabaya zaidi.”

Amesema Sudan ni mwanachama wa mikataba ya kimataifa hivyo ilinde waandamanaji badala ya kuwashambulia na itatua mkwamo unaoendelea kwa njia ya mazungumzo.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Arnold Kayanda
Sauti
1'17"
Photo Credit
United Nations