Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ufupi 04-Januari-2018

Habari kwa Ufupi 04-Januari-2018

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya maandishi ya nukta nundu ambayo hutumiwa na watu wenye ulemavu wa kutoona, Umoja wa Mataifa unapigia chepuo maandishi hayo ambayo ni njia muhimu ya mawasiliano kwa kundi hilo. Miongoni mwa wanufaika wa maandishi hayo ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria nchini Tanzania ambaye naye pia ni mlemavu wa macho na anapongeza Umoja wa Mataifa kwa kutambua na kutenga siku  ya leo ya maandishi ya nukta nundu. Na pia pongezi kwa mataifa ikiwemo Tanzania kwa kutambua kuwa maandishi ya nukta nundu ni mojawapo ya njia za mawasiliano kwa watu hususan wasioona.

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA limechukua hatua kusaidia mataifa 28 ya Afrika ambayo hayana hata mashine moja ya kutibu saratani. Lengo la IAEA ni kuhakikisha kuwa inabadili mwelekeo wa ugonjwa huo ambao mwaka 2012 kulikuwa na wagonjwa wapya 847,000 barani  humo na idadi inatarajiwa kufikia milioni 1.4 mwaka 2030.

 

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali ya Uturuki wameungana kuwafundisha stadi za kilimo zaidi ya wasyria 900 pamoja na baadhi ya wenyeji waliowapokea wakimbizi katika nchi hiyo ambayo imepokea zaidi ya wakimbizi milioni 3.5 kutoka Syria . Miongoni mwa wanufaika ni Yunus mkimbizi kutoka Syria ambaye nyumbani alikuwa mkurugenzi katika ofisi ya serikali lakini sasa ni mkulima na anasema kilimo kimemsaidia kukabiliana na ukata.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'38"
Photo Credit
© UNICEF/Pirozzi