Hii leo siku ya Ijumaa tunakuleteta Jarida mahsusi likiwa na uchambuzi wa kina wa mada moja ambayo leo ni Biashara Mtandao. Hata hivyo tunatanguliza habari kwa ufupi tukiangazia siku ya kimataifa ya nukta nundu au maandishi yanayotumiwa na watu wasioona na tumezungumza na Amon Mpanju, Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria nchini Tanzania akielezea ni umuhimu wa siku hii. Tunamulika pia wakimbizi wa Syria huko Uturuki, kutoka Ukurugenzi hadi ukulima shambani. Neno la wiki mchambuzi ni Ken Walibora na mada yenyewe ya kina inamulika Tanzania, Burundi na Kenya lakini UNCTAD nayo inafafanua kile ambacho inataka kuona, karibu na mwenyeji wako ni Arnold Kayanda.