28 Desemba 2018

28 Disemba 2018

Jaridani hii leo na Siraj Kalyango tunaanza na Sudan ambako  yaripotiwa maelfu ya watu wanaandamana kupinga ongezeko la bei za bidhaa sambamba na uhaba wa chakula na mafuta ya gari. Watoto nao waangaziwa ikielezwa kuwa mwaka 2018 ulikuwa ni mgumu zaidi kwa watoto wanaoishi kwenye maeneo ya mizozo kama DRC na Sudan Kusini. Tunamulika pia huko Rwanda ambako sera nzuri za kujumuisha wakimbizi zimeleta matumaini na ustawi siyo tu kwa wahamiaji bali pia kwa Rwanda yenyewe. Makala ni nafasi ya michezo katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs na leo Ijumaa neno la wiki BaKITA inamulika "Paraganyika." Karibu!

Audio Credit:
Siraj Kalyango
Audio Duration:
11'44"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud