Uhamiaji uzingatie utu

18 Disemba 2018

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhamiaji hii leo, Umoja wa Mataifa unasisitiza uhamiaji unaozingatia utu. Katika ujumbe wake kuhusiana na siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema  mwezi huu, dunia ilipiga hatua kwa kuidhinisha mkataba wa kimataifa wa uhamiaji salama, uliopangwa vizuri na akasisitiza kuwa ikiwa utazingatia utu, uhamiaji ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi, nguvu na ufahamu na unawaruhusu watu kutafuta fursa mpya, kunufaisha jamii wanakotoka na wanakohamia pia.

Audio Credit:
Grace Kaneiya/ Arnold Kayanda
Audio Duration:
2'28"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud