Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa Uhamiaji.

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa Uhamiaji.

Pakua

Uhamiaji ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi, nguvu na ufahamu. Uhamaji unawaruhusu watu kutafuta fursa mpya, kunufaisha jamii wanakotoka na wanakohamia pia.

Lakini uhamiaji unaporatibiwa vibaya, unaweza kuchochea mgawanyiko katika jamii, kuwaweka watu katika unyonyaji na unyanyasaji na kupunguza imani kwa serikali.

Mwezi huu, dunia ilipiga hatua kwa kuidhinisha mkataba wa kimataifa wa uhamiaji salama, uliopangwa vizuri na wa kawaida. 

Mkataba huu ukiwa unaungwa mkono na wanachama wa Umoja wa Mataifa, utatatusaidia kushughulikia changamoto halisi za uhamiaji wakati tukinufaika na faida zake nyingi.

Mkataba huo unatokana na watu na umejikita katika haki za binadamu.

Unaonesha njia za kuelekea kwenye fursa halali kwa uhamiaji na hatua madhubuti za kupambana na usafirishaji haramu wa wanadamu.

Katika siku ya kimataifa ya uhamiaji, tufuate njia iliyowekwa na azimio hili la ulimwengu ili uhamiaji unufaishe watu wote.

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
1'23"
Photo Credit
PICHA:IOM/Muse Mohammed