14 Desemba 2018

14 Disemba 2018

Leo tunaanzia nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar ambako viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja  wa Mataifa wamekutana na wanafamilia wa walinda amani 15 wa Tanzania waliouawa huko DR Congo mwaka mmoja uliopita. Tunakwenda pia huko Nairobi Kenya mkutano wa biashara mtandao ukikunja jamvi  hii leo, UNCTAD yenyewe yafunguka, tumezungumza na Dkt. Mukhisa Kituyi.  Barani Ulaya nako mkutano wa COP24 unatamatishwa kesho na leo mjumbe kutoka Tanzania ametupatia yaliyojiri, makala ni kutoka Malawi ngoma Mwinoghe yatambuliwa na Umoja wa Mataifa na kujifunza Kiswahili leo BAKITA inafafanua matumizi ya neno aghalabu! Mwenyeji wako ni Sir aj Kalyango! Karibu.

Audio Credit:
Siraj Kalyango
Audio Duration:
12'5"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud