13 Desemba 2018

13 Disemba 2018

Jaridani hii leo Siraj Kalyango anaanzia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  ambako moto umeteketeza vifaa vya uchaguzi kwenye mji mkuu Kinshasa, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo, Tume huru ya Taifa ya  Uchaguzi, CENI yazungumza. Anaangazia pia vifo vya watoto milioni 30 kila mwaka kutokana na kuzaliwa njiti au wadogo kupita kiasi na huduma duni za afya kusababisha janga hilo.  Biashara mtandao nayo ikiangaziwa huko Nairobi, Kenya, Tanzania nayo yapaza sauti. Makala ni masuala ya watu wenye ulemavu na jinsi wanavyojikwamua na mashinani ni jinsi mwanamfalme huko Nigeria alivyodhamiria kutokomeza ukeketeaji wa watoto wa kike na anatoa shukrani za dhati kwa Umoja wa Mataifa. Karibu!

Audio Credit:
Siraj Kalyango
Audio Duration:
11'40"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud