12 Desemba 2018

12 Disemba 2018

Jaridani hii leo Flora Nducha anaanza na suala la huduma ya afya kwa wote bila kujali mtu alipo,  hadhi yake na rangi yake, ananukuu ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN pamoja na mfano halisi kule Mantapala nchini Zambia, wakimbizi na wenyeji wanapata huduma ya afya eneo moja. Anakwenda hadi Uganda huko Sweden imeitikia wito wa UNICEF wa kusaidiwa ili kuweza kusambaza huduma za afya huko Magharibi mwa Mto Nile. Je umewahi kusikia 'Ukuta wa Kijani" basi unajengwa Afrika. Makala tunamsikiliza kijana Marygoreth Richard kutoka Tanzania na ujumbe wake kwa vijana na mashinani leo tunafunga safari hadi Kiribati, mradi wa Benki ya Dunia umeepusha magonjwa miongoni mwa wanakijiji wa eneo moja nchini humo. Karibu!

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
11'13"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud