Skip to main content

Kilele cha haki za binadamu na uchambuzi wa ibara ya 30!

Kilele cha haki za binadamu na uchambuzi wa ibara ya 30!

Pakua

Leo ni siku ya haki za binadamu duniani ambapo ni kumbukizi ya miaka 70 tangu kupitishwa kwa tamko hilo tarehe 10 mwezi desemba mwaka 1948  huko Paris Ufaransa.

Miaka 70 iliyopita tamko la haki za binadamu lilipitishwa, ikiwa ni  baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema kuwa kwa miaka 70, tamko la kimataifa la Haki za Binadamu limekuwa ni mhimili wa kuangaza masuala ya utu, usawa na ustawi na kuleta mwangaza wa matumaini mahala penye giza.

Azimio hilo lina ibara 30 ambapo haki zilizotajwa katika zinamuhusu kila mtu - bila kujali rangi, imani, mahali au tofauti nyingine ya aina yoyote.

Na hivyo Guterres anasema, “haki za kibinadamu ni za dunia nzima na za daima. Pia hazigawanyiki. Mtu hawezi kuchagua kati ya haki za kiraia, za kisiasa, za kiuchumi, za kijamii na za kitamaduni.”

Azimio hilo liliandaliwa kwa mchango  kutoka makundi mbalimbali ikiwemo wanawake ambao walihakikisha misingi ya kijinsia inazingatiwa.

Kwa upande wake Jebra Kambole, wakili kutoka Tanzania na mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu anatamatisha mfululizo wetu wa Ibara kwa Ibara akichambua ibara ya 30 akisema, "ibara hiyo inatoa katazo kwa mtu asipoke au kupokonya haki hizo za kibinadamu na kwamba haki hizo zinapaswa kutumika zote kama zilivyo.".

Hadi sasa nyaraka ya azimio hilo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Flora Nducah
Audio Duration
1'44"
Photo Credit
UNOG