10 Desemba 2018

10 Disemba 2018

Leo siku ya  haki za binadamu duniani, Siraj Kalyango anaanza na ripoti hiyo ikiwa pia na uchambuzi wa Ibara ya 30 ya tamko hilo ambapo Jebra Kambole mwanaharakati kutoka Tanzania anatamatisha uchambuzi wetu wa Ibara kwa Ibara, halikadhalika tunamulika huko Marrakech, Morocco mkataba kuhusu uhamiaji salama na unaofuata kanuni hatimaye umepitishwa na suala pia la biashara mtandaoni ambapo Mauritius imeibuka kidedea barani Afrika, je imefanya nini? Kulikoni imezipiku Nigeria na Afrika Kusini. Makala tunaangazia mabadiliko ya tabianchi huko Amerika ya Kusini na athari zake, bila kusahau mashinani leo ni maoni yako kutoka Facebook, karibu!

Audio Credit:
Siraj Kalyango
Audio Duration:
9'53"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud