Uganda na DRC zakubaliana kuchukua hatua kuepusha kuenea kwa Ebola mpakani mwao

5 Disemba 2018

Katika juhudi za kudhibiti mlpuko wa ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mamlaka wa mpakani nchini humo na wanzao kutoka Uganda wamekubaliana kuimarisha ufuatiliaji wa virusi vya ugonjwa huo kwa kushirikiana Zaidi. Maelezo Zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Hatua hii imefikiwa katika mkutano uliohudhuriwa na wadau mbali mbali wa afya na usalama likiwemo shirika la afya ulimwenguni (WHO) na mafisa wa afya wa wilaya za makani ambao umefanyika kwenye mpaka wa Kasindi-Luburiha, upande wa DRC.

Kuhusu ukusanyaji wa takwimu, wadau hao wamekubaliana kuoanisha matumizi ya vifaa vya kuchekecha washukiwa wa ebola na kupeana taarifa za ufuatiliaji katika maeneo haya ya mpakani.

Katika mkutano huohuo wa aina yake katika vita dhidi ya ebola mpakani, wamehaha kubaini mipaka yote inayotumiwa na wasafiri ili kutiiwe vituo vya kuwachekecha.

Kwa kutambua umuhimu wa uhamasishaji wa umaa, wamekubaliana kuhabarisha Zaidi jamii kuhusu uhalisi wa mlipuko huo na kuwaondolea Imani potofu na uvumi kuhusu virusi vya ebola.

Mafisa hao walipeana habari kuhusu uzoefu wao tangu mlipuko huo ambapo wale wa DRC, walivutiwa matumizi ya jamii katika uhamasishaji nchini Uganda.

Licha ya kutosajiliwa kwa kisa chochote cha ebola Uganda tangu mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi jirani ya DRC, imesalia chonjo na katika hatua zingine za hivi karibuni, wamechanja wahudumu wa afya wote walio msitari wa mbele kuzuia mlipuko huo kuenea hadi Uganda.

Ripoti zinasema watu Zaidi ya mia mbili walioambukizwa virusi vya ebola tangu Agosti nchini DRC, wamethibitisha kuaga dunia.

Audio Credit:
Arnold Kayanda/John Kibego
Audio Duration:
1'26"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud