UNICEF na WFP zazindua mradi wa kuboresha lishe Uganda

28 Novemba 2018

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto,  UNICEF na la mpango wa chakula, WFP wamezindua mradi wa kuboresha huduma za lishe miongoni mwa watoto katika eneo la Karamoja, kaskazini-mashariki mwa Uganda kufuatia msaada kutoka Uingereza. 

Uingereza imetoa Euro milioni 28 karibu swan a dola milioni 31.5 katika kuitikia tatizo la utapiamlo katika wilaya nane za eno la Karamoja.

Mradi huu uliozinduliwa wilayani Kotido utetekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEFT na WFP kwa kuhakikkisha kwmaba watoto na akinamama katika eneo hilo wanpata fursa ya kufikia huduma  stahiki za afya na lishe.

Dokta Doreen Mulenga ambaye ni  Mwakilishi wa UNICEF Uganda amesema msaada huu umekuja wakati mwafaka ikizingatiwa kwamab kila mmtoto mmoja kati ya watatu anadumaa kutokana na lishe duni, hivyo mradi huu ni muhimu kwa afya yao.

Ameongeza kuwa asilimia 84 ya watu wa Karamoja hawana uwezo wa  kufikia milo yenye lishe kila siku, huku asilimia 45 ya watu binafsi hswswezi kupata chakula.

Mradi huu unalenga watoto Zaidi ya 100,000 walio chini ya Umri wa miaka miano ambao wanakabiliwa na utapiamlo kupitia miredi ya lishe yua kijamii.

Utapiamlo ni changamoto kubwa katika mipango ya kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eno la Karamoja.

Karibu watoto 15,000 wanokabiliwa na utapiamlo uliokithiri watapatiwa tiba maalumu hospitalini na kwenye vituo vya afya.

Mkurugenzi wa EFP, Uganda, El-Khidir Daloum amesema wlaikuwa wametamaushwa na kiwango cha watoto wanaodumaa Karamoja ambacho kamwe hakiwezi kukubaliwa.

Audio Credit:
John Kibego
Audio Duration:
1'35"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud