Asante Tanzania lakini nyumbani ni nyumbani:Wakimbizi wa Burundi

15 Novemba 2018

Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaopata hifadhi nchini Tanzania wanaendelea kurejea nchini mwao kwa msaada wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR kufutia makubaliano maalum kati ya serikali ya Burundi na ya Tanzania yaliyofikiwa yaliyoafikiwa katika mwezi Machi mwaka huu. Kufikia sasa inakisiwa wakimbizi takriban elf 72 watakuwa wamerejea Burundi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Wakimbizi wapatao elf mbili wanaondoka kila wiki kwenye kambi tatu zilizoko magharibi mwa Tanzania na kurudi Burundi

.UNHCR imesema wakimbizi hao watapata fursa ya kuanza upya maisha yao, kutoamchango kw familia zao, jamii na pia Taifa kwa kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu yaani SDGs.Mwandishi wetu wa Maziwa makuu Ramadhani Kibuga,ameshudia ,mkoani Ruhigi, Mashariki mwa Burundi wimbi kubwa la wakimbizi wairejea nyumbani kutoka kambi ya Nduta ilioko ncini Tanzania na kisha akaanda Makala hii, ungana nae.

 

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
4'26"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud